Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Rais Magufuli ametoa kauli ikiwa ni kwa mara ya kwanza kukutana na kuzungumza na wajumbe wa Sekretarieti ya chama hicho jana mjini Dodoma ambapo amesema amepanga hatakubali mwanachama mmoja kujimilikisha mali ya chama na kuwa yake binafsi.
Mwenyekiti huyo Mpya wa Chama Cha Mapinduzi amesema kuwa atatumia madaraka aliyonayo kwa sasa katika kuhakikisha mali zote za chama zinawanufaisha wahusika wote wa chama hicho.
Dkt. Magufuli amewataka watumishi wa chama kutoa ushirikiano katika zoezi la uhakiki wa mali za Chama litakalosimamiwa na sekretarieti ya chama na ameahidi kuwa atahakikisha mapato yatokanayo na vyanzo vya mapato vya chama yanatumika ipasavyo.