Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

CHADEMA yatoa maagizo matatu kuhusu Halima Mdee

Monday , 15th Jul , 2019

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kimelaani vikali kitendo kilichofanywa na Jeshi la Polisi Mjini Bukoba, kwa kumshikilia na kumnyima dhamana Mwenyekiti wa Baraza la wanawake, Halima Mdee kitendo kinachodhaniwa kuwa ni cha kuendelea kuwanyanyasa na kuwakandamiza.

Akizungumza leo Julai 15, 2019 Mkuu wa Idara ya habari na Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini Makene, amelitaka jeshi hilo kumtendea haki Halima Mdee kwa mujibu wa sheria, na kwamba wamuachie kwa dhamana, au wampeleke mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

''Polisi wanapaswa kumfanyia mambo matatu, kumuachia huru bila masharti, kama ana makosa wamuachie kwa dhamana kwa sababu kosa lake linadhaminika, au wampeleke Mahakamani akajibu tuhuma zake kama mashtaka yake yapo. Kuendelea kumshikilia kinyume cha sheria ni jambo ambalo halikubaliki", amesema Makene.

Kwa upande wake Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya ameshangazwa na kitendo cha polisi kumkamata Halima Mdee, ilihali alikuwa anafanya kikao cha ndani cha wanawake, na kudai kuwa UWT wanafanya makongamano Kigoma.

Halima Mdee alikamatwa Julai 14, mara baada ya kumaliza kufanya kikao cha ndani cha kuwajengea uwezo wanawake wapya waliochaguliwa katika baraza hilo, anashikiliwa katika kituo cha Polisi Bukoba kwa kosa la kutoa maneno ya uchochezi.

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya