Tuesday , 13th Dec , 2016

Halmashauri kuu ya Taifa ya Chama cha Mpinduzi CCM imeagiza kuundwa kwa kamati maalum ya kufanya tathmini ya kina kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar kwa ujumla na masuala yanayohusu uchaguzi wa Zanzibara 2015.

Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Magufuli akiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana

 

Hayo yamesemwa na mkuu wa idara ya itikadi na uenezi wa chama chja mapinduzi CCM Mheshimiwa Nape Nnauye wakati akiwasilisha mapendekezo yaliyotolewa na halmashauri kuu ya taifa ya CCM iliyokutana tarehe 13.12.2016 Jijini Dar es salaam kwa muda wa siku moja,kikao kilichoongozwa na Mwenyekiti wa taifa wa CCM Dkt.John Pombe Magufuli.

Amesema mwenyekiti wa kamati ya udhibiti na nidhamu ametakiwa akamilishe kazi ya taarifa ya udhibiti kwa wanachama waliokiuka mienendo ya kiuanachama kabla ya kuanza uchaguzi mkuu wa chama mwezi Februari 2017, mikoa na wilaya ambazo hazijapeleka taarifa zao za kiudhibiti ziwe zimefikisha taarifa zao kwa mwenyekiti wa kamati wa udhibiti na nidhamu kabala ya tarehe 30.01.2017.

Nape Nnauye

Sanjari na hilo amesema uhakiki wa mali za chama unaendelea kufanyika kwa kina na uchambuzi zaidi ukikamilika taarifa yake itawasilishwa kwa sekretarieti ya halmashauri kuu ya taifa mapema iwezekanavyo.

Aidha ameongeza kuwa maamuzi na mapendekezo hayo yatapelekea kufanyika kwa mabadiliko ya katiba ya chama na kanuni za Jumuiya za chama.