Ester Bulaya Mbunge wa Bunda Mjini
Akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio, Mh. Sokombi amesema presha ya Ester Bulaya ambaye ni Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini bado ipo chini, kiasi kwamba wameshindwa kumsafirisha kwenda hospitali kubwa, hivyo wanasubiri madaktari wamsaidie kurudisha hali ya presha yake, ndipo wamtoe hospitali.
Pia Mh. Sokombi amesema kwa sasa Bulaya ameshapatiwa dhamana akiwa hapo hospitalini, lakini hawajajua hatma ya kesi kwani mpaka sasa hawajapewa maelezo ya sababu iliyofanywa ashikiliwe na polisi.
Msikilize hapa akielezea kwa kina zaidi juu ya jambo hili.