Rais Magufuli
Kamishna Mkuu Rogers William Sianga atasaidiwa na Bw. Mihayo Msikhela ambaye anakuwa Kamishna wa Operesheni na Bw. Fredrick Kibuta ambaye anakuwa Kamishna wa Intelijensia.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Anna Peter Makakala kuwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Anna Peter Makakala alikuwa Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji Moshi, kilichopo Mkoani Kilimanjaro.
Uteuzi huu unaanza mara moja na wateule wote wataapishwa Jumapili tarehe 12 Februari, 2017 saa 5:00 Asubuhi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Hatua hii ya Rais Magufuli inaweza kuwa ni utekelezaji wa ushauri uliotolewa wiki iliyopita bunge na Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya.
Mtazame hapa...