Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Tanzania, DCP Mohamed Mpinga Pichani
Kamanda Mpinga ametoa takwimu hizo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wadau wa usafirishaji nchini kwa lengo la kuweka na kupanga mikakati itakayosaidia kupunguza ajali za barabarani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea siku kuu za mwisho wa mwaka.
Amesema kuwa kwa wakati mwingine wananchi ndiyo chanzo cha ajalli hizo kwa kushabikia mwendo kasi wa madereva wanaovunja sheria za usalama barabarani kwa kisingizio cha kuwahi waendako.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mdhibiti wa Usafiri wa Reli kutoka Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na nchi Kavu (SUMATRA) Dk. Michael Kisaka amesema kuwa wameweka mabalozi kwa kila basi kutoka vituo vikubwa vya mabasi ya abiria kwa ajili ya kutoa elimu ya bure kwa abiria na kugawa sheria za usalama barabarani.