CCM yawaonya wanaotangaza nia ya kuwania urais
Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi nchini Tanzania CCM imewatahadharisha wanachama wake walioonesha nia ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kuwa wanaweza wakapoteza sifa za kugombea nafasi hiyo.

