Tanzania yaanza kujipanga kuelekea UNGASS2016
Tanzania imeandaa kongamano ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ushiriki wa nchi kwenye kikao maalum cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu tatizo la madawa ya kulevya duniani, UNGASS2016 kitakachofanyika mwezi Aprili mwaka huu nchini Marekani.
