Runinga zatakiwa kuweka wakalimani lugha za alama
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri mkuu anayeshughulikia walemavu nchini Tanzania Dkt. Abdalla Posi amevitaka vyombo vya habari nchini kuweka watafsiri wa lugha ya alama katika Luninga ili kuwasaidia watu wenye ulemavu kupata taarifa.
