Hatuwaogopi Wamisri, kesho tutawafunga - Samatta
Nahodha wa timu ya taifa Taifa Stars Mbwana Samatta amesema licha ya mechi ngumu inayowakabili hapo kesho dhidi ya Misri, lakini hawawezi kuingia Uwanjani kwa kuwaogopa kwa sababu ni timu kubwa bali wataingia kwa ajili ya kutafuta ushindi.