Serikali yakanusha taarifa za jarida la Uingereza
Serikali imesema kumekuwa na ongezeko la miradi ya uwekezaji katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya utawala wa rais Dkt. John Pombe Magufuli, tofauti na ilivyoripotiwa na jarida la The Economist la nchini Uingereza kwamba uwekezaji umepungua.