Jumanne , 5th Jul , 2016

Klabu ya Barcelona imemrejesha kiungo Denis Suares kutoka katika klabu ya Villarreal kwa mkataba wa miaka minne.

Suarez mwenye umri wa miaka 22 na kiungo wa timu ya taifa ya Hispania amerejea Barcelona kwa dau la paundi milioni 2.7.

Luis Enrique alijaribu kumleta Suarez Barcelona mwezi Januari lakini kiungo huyo alikubali kukaa Villarreal mpaka mwisho wa kampeni.

Suarez atafanyiwa vipimo vya afya leo na atatangazwa rasmi kujiunga na klabu huyo kesho.

Chanzo BBC