Cheka mdogo kuwania UBO kesho dhidi ya Mmalawi.
Bondia Mtanzania Cosmas Cheka kesho anapanda ulingoni Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam kupambana na bondia kutoka nchini Malawi, Chrispin Moliyati katika pambano la kuwania ubingwa wa Universal Boxing Union (UBO) wa uzito wa Super Feather.