Cheka ulingoni kupambana na Mmalawi leo
Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Cosmass Cheka leo anapanda ulingoni Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam kupambana na bondia wa Malawi, Chrispin Moliyati katika pambano la kuwania ubingwa wa UBO wa uzito wa Super Feather.