Tiboroha asema wanasubiri barua rasmi ya TFF.
Uongozi wa Stand Utd kampuni bado unasubiri barua ya maamuzi yaliyotangazwa na shirikisho la soka nchini TFF kupitia kamati yake ya uchaguzi ambayo ilikwenda Mkoani Shinyanga kukutana na pande mbili za klabu hiyo ambazo zilikuwa zikivutana.
