Serikali yasisitiza ujenzi wa viwanda
Serikali imeahidi kuendelea kusimamia ahadi ya kuwa na serikali ya viwanda ili kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2020, mchango wa viwanda katika pato la taifa unakuwa mpaka kufikia asilimia 15 kutoka kiwango cha sasa cha asilimia 7.3 kwa mwaka.