Yanga kuufikisha 'ubingwa wa Simba' mahakamani
Mabingwa watetezi wa Tanzania Bara Yanga SC wamesema hawana imani na kamati iliyoundwa ya saa 72 ya kuchunguza rufaa ya Simba SC kwa Kagera Sugar kwa kuwa imeshaanza mipango ya kuchakachua ripoti ya mwamuzi kwa lengo la kusaka ushindi wa mezani.

