Madrid yamteua kipa wa zamani wa Barcelona
Baada ya wiki kadhaa kupita tangu aliyekuwa kocha mkuu wa klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid, Mfaransa Zinedine Zidane kuachia ngazi hatimaye timu hiyo imemtangaza kocha wa Hispania Julen Lopetegui kuziba nafasi yake.