Mstaafu mwingine aingilia sakata la Spika na CAG
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Pius Msekwa amesema kwa mujibu wa sheria ya Bunge Spika, Job Ndugai ana mamlaka ya kumuuita kiongozi yeyote kwa mujibu wa sheria endapo atakiuka taratibu na sheria za kibunge.

