Yanga na Simba matatani kwa ushirikina uwanjani
Shirikisho la soka nchini (TFF) kupitia kwa Bodi ya Ligi (TPLB) na kamati ya saa 72, imevitaka vilabu kutojihusisha na vitendo vya kishirikina kama ambavyo vimejitokeza hivi karibuni kwenye mechi mbalimbali zikiwemo zilizohusisha Simba na Yanga.