Sijahusika na mauaji Bangladesh - Sheikh Hasina
Waziri mkuu wa zamani wa Bangladesh Sheikh Hasina amekanusha kutenda uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa msako mkali dhidi ya maasi ya mwaka jana yaliyomuondoa madarakani, siku chache kabla ya mahakama maalum inayomkabili kutoa uamuzi.

