Ujumbe wa Rais Magufuli baada ya kuingia 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia Watanzania wote heri ya Mwaka mpya wa 2020 na kuwaomba waendelee kudumisha amani na upendo ili uwe mwaka wa maendeleo na ustawi kwa Taifa.