DC agawa Mahindi kwa wananchi ili wajisajili NIDA
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga Anamringi Macha, amesema kuwa aliamua kugawa Mahindi pamoja na Ndizi mbivu kwa wananchi wake, waliokuwa wamepanga foleni ya kupata namba za utambulisho wa Taifa kutoka NIDA kwa lengo la kuwafundisha uvumilivu na kutokata tamaa katika zoezi hilo.

