Wizara yazungumzia kuhusu vikwazo vya Marekani
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imesema kuwa hadi sasa hivi haijapokea waraka wowote wa Kidplomasia kutoka nchini Marekani, unaoeleza kuwa Nchi ya Tanzania ni miongoni mwa Nchi ambazo zitawekewa vikwazo kwa raia wake kwenda nchini Marekani.

