Walimu wakimbia makazi kisa kupigwa, kulazwa nje
Walimu wanaofundisha katika shule mbalimbali zilizopo katika Halmashauri ya Mji wa Geita, wamelazimika kukimbia makazi yao kwenye maeneo ya shule kutokana na kuchapwa mijeredi na wakati mwingine kujikuta wakiwa wamelazwa nje.