Ndalichako atoa siku tatu kwa vyuo vikuu nchini
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako ametoa muda wa hadi kufika Ijumaa wiki hii ambayo itakuwa Juni 5, 2020, vyuo vyote vya elimu ya juu hapa nchini viwe vimemaliza kuwapa fedha za kujikimu wanafunzi wote na si vinginevyo.