"Hakuna Mbunge aliyeripoti" - Mambosasa
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa amesema kuwa mpaka sasa hivi hakuna Mbunge yeyote aliyeripoti kwenye ofisi ya Mpelelezi wa kanda hiyo, kutokana na kukiuka kwa agizo la Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda, aliyewapa masaa 24 kurudi Bungeni.