Kauli ya Kubenea baada ya kuhamia ACT Wazalendo
Aliyekuwa Mbunge wa Ubungo kupitia CHADEMA Saed Kubenea, amesema kuwa maamuzi ya yeye kujiunga rasmi na chama cha ACT Wazalendo yalikuwa ni magumu, kwa kuwa hicho ndiyo chama chake cha pili kujiunga tangu aanze siasa na kudai kuwa ndani ya Jiji la Dar es Salaam upinzani una nguvu kubwa.

