Jumatano , 3rd Jun , 2015

Staa wa Shilole baada ya sakata lake la kusambaa kwa picha zinazoonesha sehemu ya maungo yake ya siri hadharani akiwa katika onesho huko Ubeligiji, hatimaye amejisalimisha BASATA kujieleza na kusamehewa rasmi kwa kosa alilofanya.

msanii wa muziki wa bongofleva nchini Shilole

Shilole, maarufu zaidi kama Shishi Baby ameweka wazi taarifa hizo kwa mashabiki wake kuwaweka sawa, hasa pia baada ya taarifa kutoka kwa BASATA na tamko la Serikali Bungeni kuwa atachukuliwa hatua.

Kuhusiana na hili tumeongea na Shilole ambaye hapa anafafanua kilichotokea.