Jumatano , 27th Mei , 2015

Wasanii wa muziki wa kimataifa, Yasin Bey maarufu zaidi kama Mos Def na Talib Kweli wanatarajia kuwajengea wasanii kutoka Afrika Mashariki hamasa na pia jukwaa la kuonesha vipaji vyao, kupitia onesho kubwa kabisa ambalo watafanya huko Kenya hii leo

Talib Kweli | DJ | Mos Def

Kwa kushirikiana na wasanii kutoka Kenya, mastaa hawa pia watashiriki katika mjadala kuhusu namna ya kuipeleka mbele Hip Hop ya Kenya, vilevile kutangaza vipaji vinavyopatikana nchini humo na kutengeneza mahusiano kati ya wasanii wa ndani na wale kutoka nje ya mipaka.

Wasanii kutoka Kenya ambao watashiriki katika tukio hilo ni pamoja na Wangechi, Xtatic, Rabbit, Bamboo kati ya wengine.