Akizungumza na East Africa Radio, Afisa Habari wa timu hiyo, Costantine Masanja amesema, wamewapa wachezaji wao likizo ya mwezi mmoja kwa ajili ya kupumzika lakini wanaingia kambini mapema ili kufanya maandalizi mazuri kwa ajili ya kujiandaa na ligi hiyo yenye ushindani mkubwa.
Masanja amesema, katika msimu uliopita hawakufanya vizuri lakini wanaamini msimu ujao watafanya vizuri kwani mazoezi yataanza mapema ikiwa ni pamoja na kuwapima wachezaji ambao wapo nao kwa ajili ya majaribio.
Masanja amesema, kocha Fredy Minziro ameshakabidhi ripoti yake na sasa wapo katika mikakati ya kuitekeleza.