Jumamosi , 23rd Mei , 2015

Staa wa muziki Quick Rocker, ameweka wazi mchango mkubwa sana wa msanii Barnaba katika ngoma yake mpya ya Beautiful, akieleza kuwa msanii huyo ndiye aliyeandika na vilevile kuitengeneza (production) ya rekodi hiyo kali kwa sehemu kubwa.

Quick Rocker

Quick Rocker amesema anamshukuru sana Barnaba kwa mchango huo, akieleza kuwa rekodi hiyo imefanyika katika studio mbili tofauti, ikiwepo ile ya Switcher ambayo ndiyo anayoimiliki na pia studio ya msanii Barnaba.

Star huyo wa michano na vilevile kuimba, amesema kuwa, rekodi hiyo ambayo ameimba ndani yake inaendeleza kuonesha upande wake wa pili wa kuimba, pembeni ya kurap, ujumbe mkubwa ndani yake ikiwa ni kukubali mchango wa wanawake ambao wana nafasi kubwa katika kuitunza, kuleta furaha na kuendeleza jamii.