Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Gallawa.
Akikabidhi msaada huo kwa mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Gallawa, meneja wa Kanda wa benki ya NMB, Gabriel Ole Loibanguti alisema msaada huo ni sehemu ya benki hiyo kutoa faida inayoipata kwa ajili ya kuhudumia jamii.
Alisema kuwa kwa kipindi cha mwaka 2015 Benki hiyo imetenga jumla ya Tsh 1 bilion kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali za kijamii.
Akitoa shukrani zake baada ya kukabidhiwa msaada huo Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Dk, Zainabu Chaula alisema kuwa hospitali hiyo ina upungufu wa magodoro 422 hivyo kwa msaada huo uliotolewa hospitali hiyo bado ina uhitaji wa magodoro 400 na kuwataka wadau mbalimbali wa sekta ya afya mkoani Dodoma kuwasaidia.