Akizungumza na East Africa Radio, Mratibu wa mashindano hayo, Paul John amesema, mchezo wa mieleka unahitaji nguvu na una kanuni na sheria tofauti hivyo ni vizuri kuwafundisha vijana wadogo ili wazijue na kuwa msaada kwa miaka ijayo.
John amesema, michezo mingi imekwama kuendelea nchini kutokana na wachezaji wengi kuibukia ukubwani na kushindwa kujua miiko inayotakiwa ndio maana huwa wanafanya vibaya kwenye mashindano mbalimbali ambayo huandaliwa na ngazi za mikoa ama taifa.