Jumatatu , 27th Apr , 2015

Msanii wa muziki wa injili Ester Wahome kutoka nchini Kenya, katika moja ya mafanikio yake makubwa katika shughuli za muziki anaofanya, mapokezi mazuri aliyopata huko nchini Burundi, ikiwepo kukutana na Rais wa nchi hiyo.

mwimbaji wa muziki wa nchini Kenya Ester Wahome

Sambamba na nafasi hiyo kubwa, katika ziara yake nchini humo, Ester ameweza kufanya maonyesho mawili makubwa ambayo yote yaliweza kuhudhuriwa na wanasiasa wakubwa wa nchi hiyo, na hivyo kumtia moyo sana msanii huyo katika safari yake ya kisanaa.