Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh, Mathius Chikawe.
Akiongea na Waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh, Mathius Chikawe amesema ulinzi huo umeimarishwa kutokana na taarifa zilizosambaa kuwa kikundi cha kigaidi cha Al shaabab kinalenga kushambulia mikoa ya Arusha, Mbeya, Mwanza na Dar es Salaam.
Aidha Mh. Chikawe amewataka wazazi na walezi nchini kuweza kuangalioa mienendo ya watoto wao ili wasiweze kujiunga na makundi ya kihalifu ikiwemo ugaidi akitolea mfano mtoto aliekamatwa akijihusisha na ulipuaji katika chuo Garissa nchini Kenya.
Chikawe amesema kuhusu kukamatwa kwa Rais huyo wa Tanzania, Rashid Mberesero kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo la mashambulizi katika chuo kikuu cha Garissa amesema serikali haijapewa taarifa rasmi kuhusiana na mtuhumiwa huyo.
Katika hatu nyinginr Waziri huyo amesema kuwa kwa sasa ili kuiweka nchi katika usalama zaidi kila mgeni anaeingia nchini wizara hiyo ina taarifa zake na wanaoingia kinyume cha sheria kurudishwa nchini kwao.