Katika taarifa yake, Msemaji wa Azam FC Jaffar Idd Maganga,amesema Kavumbagu yuko Tanzania kwa sababu ya uzembe wa Shirikisho la Soka Burundi.
Maganga amesema, amesema shirikisho hilo liliwasiliana na uongozi wa Azam FC likimuomba Kavumbagu kwa ajili ya kuitumikia timu yake ya taifa katika mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA mwishoni mwa wiki hili tangu wakiwa Khartoum, Sudan wakicheza dhidi ya El-Merrikh, lakini mkali huyo wa mabao amekwama kwenda kutokana na kutotumiwa tiketi ya ndege.
Maganga amesema, wameshangazwa na taarifa zinazoenezwa kwamba tumemzuia Kavumbagu kwenda kuitumikia timu yake ya taifa na hili linaonyesha kuwachafua kimataifa.
Maganga amesema Mchezaji anaruhusiwa na klabu yake kwenda kuitumikia timu ya taifa pale shirikisho linapokuwa limetuma tiketi kwa klabu husika ambapo tiketi ya Kavumbagu kwenda kuitumikia timu yake ya taifa si jukumu la Azam FC.
Kavumbagu, mchezaji wa zamani wa Atletico FC ya Burundi na Yanga SC, ameifungia Azam FC mabao 10 katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu ikiwa ni bao moja nyuma ya kinara, Simon Msuva wa Yanga SC.