Ijumaa , 27th Mar , 2015

Klabu ya Simba imesema inaamini mbio za kuelekea kuchukua Ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara upo na wanaamini watashinda kutokana na kikosi hicho kuwa na ushirikiano na kujiamini wawapo uwanjani.

Akizungumza jijini Dar es salaam, mkurugenzi wa kitengo cha habari cha timu hiyo, Haji Manara amesema mbio za ubingwa wa ligi ni sawa na Riadha na mpaka sasa hamna ambaye aliyefikia alama za mwisho au aliyemaliza ligi.

Manara amesema, mpaka sasa Timu bado haijakata tamaa na haiwezi kukata tamaa kwa sababu bado nafasi ya kuibuka na ubingwa wa ligi kuu Soka Tanzania Bara wanayo.