
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema ajali ya treni ya SGR iliyotokea katika eneo la Ruvu Mkoani Pwani asubuhi ya leo Oktoba 23, 2025 wakati ikitokea Jijini Dar es salaam kuelekea Dodoma imesababishwa na hitilafu za kiuendeshaji ambazo zilipelekea mabehewa matatu (3) kuacha njia.
Ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 2;00 asubuhi na hakuna aliyejeruhiwa licha ya hofu iliyowapata abiria wachache kufuatia ajali hiyo.
Taarifa ya TRC imeeleza kuwa timu ya wataalamu ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Uchukuzi, Mkurugenzi Mkuu TRC na vyombo vya usalama na menejimenti ya TRC wanaendelea na uchunguzi wa kina sambamba na kuhakikisha huduma zinarejea kwa haraka.