Alhamisi , 3rd Jul , 2025

Rais Donald Trump wa Marekani atakutana na viongozi kutoka mataifa matano ya Afrika mjini Washington wiki ijayo, kujadiliana 'fursa za kibiashara

Trump atakutana na viongozi wa Gabon, Guinea-Bissau, Liberia, Mauritania na Senegal kwa majadiliano na chakula cha mchana siku ya tarehe 9 katika Ikulu hiyo.

Afisa mmoja wa Ikulu ya White House amesema Trump anaamini kwamba nchi za Kiafrika zina fursa kubwa za biashara, ambazo zina manufaa kwa watu wa Marekani na washirika wao barani Afrika.

Tangu aingie madarakani, Trump amechukuwa hatua kadhaa zinazoathiri mahusiano yake na mataifa ya Kiafrika, ikiwemo kupunguza misaada kwa kiwango kikubwa. #EastAfricaRadio