Jumamosi , 28th Jun , 2025

Utafiti uliochapishwa katika #ArchivesOfBehavior umebaini kuwa wanaume wenye ndevu wana uwezekano mkubwa wa kudumu katika mahusiano ya muda mrefu badala ya kutafuta wapenzi wapya.

Katika utafiti huo uliowahusisha mamia ya wanaume wenye umri kati ya miaka 18 hadi 40, watafiti waligundua kuwa wale waliokuwa na ndevu nyingi walionyesha motisha kubwa ya kutunza uhusiano wao wa sasa na kuwajali wanafamilia, tofauti na wale waliokuwa wakinyoa ambao walionekana kuwa na mwelekeo wa kutafuta wapenzi wapya.

 

Profesa Peter Jonason kutoka Chuo Kikuu cha Cardinal Stefan Wyszynski, Warsaw, alisema kuwa jitihada na muda unaohitajika kutunza ndevu huweza kuwa ishara ya nidhamu na kujitolea kwa ajili ya utulivu katika maisha.