
Katika utafiti huo, washiriki walilazimika kulala kwa saa nne tu kwa kila usiku kwa siku mbili mfululizo. Baada ya majaribio hayo, washiriki waliripoti kuwa walijihisi kuwa wazee kwa wastani wa miaka 4.44 zaidi ya umri wao halisi.
Kwa upande mwingine, walipopewa muda mrefu wa kulala – saa tisa kwa kila usiku kwa siku mbili mfululizo – washiriki waliripoti kuhisi kama wamepungua umri kwa takribani miezi mitatu ikilinganishwa na umri wao.