Jumanne , 15th Apr , 2025

Promota Bob Arum anaamini Tyson Fury hatarejea tena kwenye masumbwi baada ya bondia  huyo kutangaza kustaafu Januari mwaka huu.

Promota Bob Arum na Tyson Fury

Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 36 alifanya uamuzi huo wa kushtukiza wiki chache tu baada ya kupigwa  mara mbili mfululizo na bingwa wa WBA (Super), WBC na WBO Oleksandr Usyk.

"Kama ningekuwa mtu wa kamari ningebeti kwa kusema hatapigana tena” Bob Arum

Fury amestaafu zaidi ya mara moja katika mchezo wa masumbwi akiwa na rekodi ya kushinda mara 34, sare moja na kupigwa mara mbili dhidi ya Oleksandr Usyk aliyeharibu rekodi yake ya kucheza miaka 15 bila kupoteza pambano lolote.