Jumanne , 4th Mar , 2025

FA ya nchini England inafikiria kumfungia kwa muda mrefu mlinda mlango wa Millwall Liam Roberts kutokana na faulo aliyomchezea nyota wa Crystal Palace Jean-Philippe siku ya Jumamosi klabu hiyo ya EPL ilipo tinga robo fainali ya FA kwa ushindi wa 3-1

Liam Roberts akimfanyia foul Jean-Philippe

Mlinda mlango huyo alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kumjeruhi Mateta ambaye alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia katika sikio la kushoto  na kukimbizwa hospitalini ambapo  ameshonwa nyuzi 25 katika jeraha hilo

Baada ya kadi hiyo nyekundu Roberts atakosa michezo mitatu ukiwepo mchezo wa  kesho timu hiyo inayoshika nafasi ya 12 ya Championship itakapokutana na  na  Bristol City