Ijumaa , 28th Feb , 2025

Baada ya sakata la TikTok nchini Marekani kupamba moto moja kati ya kitu ambacho kilikuwa kinazungumzwa sana ni 'Meta' kuja na suluhisho kwa kutengeneza Application ambayo itakuwa na mfanano kama TikTok kimatumizi.

Lakini kwa sasa suala la Meta kulifanya wazo hili kuwa uhalisia limeonekana kuchukua sura mpya, na hii ni baada ya tetesi zinazosemekana kwamba wamepanga kuifanya 'Reels' ile ya Instagram kuwa Application ambayo inajitegemea.

Chanzo ambacho hakikupenda kujulikana anasema alimsikia Adam Mosseri ambaye ni mkuu wa Instagram akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo kuhusiana na wazo hili, na lengo ni kuifanya Reels kuwa na vitu vingi zaidi ikiwemo uwezo wa kuweka video zenye dakika 3 kuendelea na kumfanya mbunifu kufurahia zaidi kutengeneza maudhui kwenye mtandao huo.

Kwa sasa kinachofanywa na mtandao wa Instagram ni kuwalipa baadhi ya Creators ili kufanya promotion kuhusu mtandao wa Instagram kwenye Application nyingine kama vile Snapchat na TikTok na wamepanga pia kuahidi pesa nyingi kwao ikiwa creators hao watakubali kuweka maudhui yao kwenye Application mpya ya Reels (exclusive content)

Chanzo: reuters