Jumanne , 25th Feb , 2025

Taarifa ya Vatican imeeleza kuwa hali ya Papa Francis imeendelea kuimarika na changamoto ya kupumua ambayo ilitokana na homa ya mapafu haijajitokeza tena, huku akiwashukuru watu wote duniani ambao wamekuwa wakimuombea tangu aanze kuugua.

Papa Francis

Taarifa ya usiku wa kuamkia jana Februari 24, 2025, imeeleza kwamba hata tatizo la awali la figo lililogunduliwa halijaleta mabadiliko mabaya hadi sasa.

Papa Francis mwenye umri wa miaka 88 yuko katika hospitali ya Gemelli mjini Roma, ambapo anapatiwa matibabu katika chumba chake maalum kwa zaidi ya wiki moja sasa.

Aidha matibabu ya oksijeni yanaendelea ingawa si kwa kiwango kile kikubwa kilichokuwa kikitumika hapo mwanzo.