Ijumaa , 21st Feb , 2025

Droo ya hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa barani Ulaya imepangwa mchana wa leo ambapo bingwa mtetezi wa michuano hiyo Real Madrid amepangwa kucheza na mpinzani wake wa Laliga Atletico Madrid 

Droo ya hatua ya 16 bora UEFA

Kwa Upande wa Liverpool ambao waliongoza kwa kukusanya alama kwenye hatua ya ligi wao watavaana na matajiri wa Ufaransa PSG, huku Barcelona ikipangwa kuvaana na Benfica ya Ureno

Kwa upande wa wababe wa Italy Inter Milan wao wamepangwa  kucheza na Feyenoord, Borussia Dortmund watacheza na Lille, wakati Club Brugge akivaana na Aston Villa

Miamba ya Ujerumani Bayern Munich wao watacheza na bingwa mtetezi wa Bundesliga Bayer Leverkusen na Mechi nyingine PSV watakabiliana na Arsenal