Jumatano , 29th Jan , 2025

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania (LHRC), kimetoa wito kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kushiriki kwenye uchaguzi mkuu wa nchi hiyo hata kama madai yao ya Katiba mpya na mabadiliko kwenye mfumo wa uchaguzi hayatofanyiwa kazi na serikali

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania (LHRC), kimetoa wito kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kushiriki kwenye uchaguzi mkuu wa nchi hiyo hata kama madai yao ya Katiba mpya na mabadiliko kwenye mfumo wa uchaguzi hayatofanyiwa kazi na serikali.

Wito huo wa LHRC unafuatia msimamo uliotangazwa na mwenyekiti mpya wa CHADEMA Tundu Antipas Lissu kuwa chama hicho hakitoshiriki kwenye uchaguzi huo wa mwezi oktoba kama matakwa yao yatapuuzwa