Ijumaa , 17th Jan , 2025

Wavuti ya kujifunza lugha mtandaoni inayofahamika kama Duolingo, imetoa takwimu zinazoonyesha kuwapo kwa ongezeko kubwa la idadi ya watu wanaojifunza Mandarinnchini Marekani, idadi ambayo ni kubwa ukilinganisha na miaka mingine.

 

Hii Mandarin ni lahaja ndani ya lugha ya kichina na ndiyo ambayo inaonekana kuwa bora na inayotumika kwenye mji mkuu wa China, Beijing. sasa unaweza kujiuliza ni kwa nini wamarekani wanajifunza kichina kwenye nyakati kama hizi.

Jibu ni kwamba baada ya tetesi za kufungiwa kwa mtandao wa TikTok nchini humo, idadi kubwa ya watumiaji wa mtandao wa TikTok wameonekana wakihamia kwenye mtandao wa RedNote. RedNote ni mtandao ambao kimsingi unamilikiwa na China, na lugha kubwa inayotumika kwenye mtandao huo ni kichina.

Ilivyo RedNote ni kama TikTok tu, hapo sasa umepata mwanga wa kwa nini kuna idadi kubwa ya watu wanaojifunza lugha ya kichina nchini Marekani kwa sasa