Jumatano , 27th Nov , 2024

Kada wa CHADEMA Stephano Evaristo Chalamila mwenye umri wa miaka 23 ambaye pia ni ofisa wa chama Kata na mkazi wa kijiji cha Chapwa A wilaya ya Momba mkoani Songwe, ameuawa usiku wa kuamkia leo Novemba 27, 2024, baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana nyumbani akiwa amelala na kukatwa

Bendera

na kitu chenye ncha kali kichwani na mkononi.

Mwenyekiti wa baraza la wazee jimbo la Tunduma Ally Mwafongo, amesema kuwa marehemu ambaye ni afisa wa chama kata alivamiwa nyumbani kwake majira ya usiku na kuchalangwa na vitu vyenye ncha kali.     

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe SACP Agustino Senga, amesema hadi sasa wanamshikilia mtu mmoja ambaye ni bodaboda kwa ajili ya mahojiano ili kujua chanzo cha tukio hilo pamoja na wale waliohusika.